Vanessa Mdee Kaachiwa Kwa Dhamana
Mwanamuziki
Vanessa Mdee maarufu Vee Money ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuwa ameshikiliwa kwa takribani
wiki moja kufuatia tuhuma ya dawa za kulevya inayomkabili.
Mdee
aliachiwa jana jioni ambapo anatuhumiwa kutumia na kusambaza dawa za
kulevya. Alishikiliwa na Polisi tangu juma lililopita baada ya kwenda
kuripoti kufuatia kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa hizo
iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam, Paul Makonda.
Post a Comment