Baada ya Kuitungua KMC, Yanga Yarejea Dar
KIKOSI cha Yanga kimetua saa 4:00 asubuhi hii kikitokea Songea mkoani Ruvuma kwenye mchezo wa ligi dhidi ya KMC na kuunganisha moja kwa moja kuhani msiba wa mchezaji mwenzao.
Yanga jana walikuwa ugenini dhidi ya KMC kwenye uwanja wa Majimaji na kufanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0 ukiwa ni mchezo wao wa tatu kukusanya pointi zote tatu baada ya Kagera Sugar kuifunga bao 1-0 na Geita Gold bao 1-0.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingiza anasema wanashukuru kupata pointi tisa kwenye michezo yote waliyocheza na wanaahidi kuendeleza ushindi kwenye michezo iliyombele yao.
“Msimu uliopita ni kweli tulianza vizuri lakini tukashindwa kuwa na mwendelezo mzuri msimu huu kikosi chetu ni bora na kinabadirika kadri siku na mechi zinavyochezwa hivyo hatutarajii kurudia yaliyopita,” anasema.
Akizungumzia kwenda kuhani msiba Temeke alisema mchezaji Paul Godfrey ‘Boxer’ ameondokewa na mzazi wake hivyo kama familia wameona umuhimun wa kwenda kumpa pole na kumsindikiza mzazi wao kwenye nyumba ya milele.
“Boxer ni Yanga amepata shida hatuwezi kumuacha peke yake kwenye kipindi hiki kigumu anachokipitia ni jambo jema tukaungana naye ili kumfariji,” anasema.
Post a Comment