IRENE UWOYA ADAI HAVUTIWI NA WANAUME WENYE MIONEKANO MIZURI
Iko wazi, katika ile list ya wasichana warembo kutoka kwenye kiwanda cha Bongo Movie huwezi kusahau kumtaja Irene Uwoya, hii ni kutokana na yeye alivyojiweka kwenye suala zima la urembo wake au uzuri wake na kumfanya kutoshuka wala kupanda.
Muigizaji huyo ambaye ameandaa event maalum kwaajili ya Valentine’s Day aliyoipa jina, ‘Irene Uwoya Valentine’s Special Night,
ameahidi kueleza baadhi ya mambo ambayo watu hawafahamu kuhusu yeye
katika sekta ya malavidavi. Leo Feb 8, Irene kanyoosha maelezo juu ya
kile anachokiamini hasa katika suala zima la mahusiano.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, ameandika.. “Kitu
ambacho hamkijui kuhusu mimi ni kuwa SIJAWAHI kuvutiwa na wanaume wenye
mionekano mizuri, sielewi ni kwanini lakini wanaume wenye sura mbaya
huwa wanaamsha hisia zangu za KIMAPENZI”
Kuelekea
siku ya Valentine, kwa mujibu wa muigizaji huyo atakuwa akitoa fact
moja moja kila siku ambazo tulikua hatuzijui kutoka kwake, na kwa fact
hii ya kwanza inaweza kuamsha ari kwa wanaume waliokua wanaamini wana
mionekano isio mizuri nao kujiona wako kwenye kundi la kupendwa na
warembo.
Post a Comment