Madai: Wema Apelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali
Taarifa zilizotufikia zimeeleza kuwa, msanii wa Bongo Movie,
Wema Sepetu hajafikishwa mahakamani Kisutu leo kwa madai kuwa amepelekwa
kwa Mkemia Mkuu wa Serikali leo kwa ajili ya kupimwa na kuthibitisha
iwapo anatumia madawa ya kulevya au la!
Imedaiwa kuwa, Polisi Dar, wamefikia hatua hiyo baada Wema kukana kutumia madawa wakati alipokuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.
Imedaiwa kuwa, Polisi Dar, wamefikia hatua hiyo baada Wema kukana kutumia madawa wakati alipokuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi.
Taarifa zimedai kuwa mastaa wenzake kama TID na wengine walikiri
kutumia madawa na kupewa onyo kali huku mahakama ikiwapa masharti matatu
likiwemo la kuripoti polisi mara mbili kwa mwezi ndani ya mwaka mmoja
na kuwa chini ya uangalizi wa mahakama, kisha kujidhamini kwa bondi ya
shilingi milioni moja na kurudi uraiani wakati Wema akikana kutumia
madawa.
Taarifa zaidi zimedai kuwa, polisi wanaendelea kumshikilia Wema huku
wakisubiri ripoti ya mkemia mkuu ili waweze kukamilisha upelezi na
kumchukulia hatua zinazostahili.
Post a Comment