Sakata la Madawa: Kauli ya Chadema Baada ya Makonda Kumtaja Mbowe
DAR ES SALAAM: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema muendelezo wa kukamatwa kwa viongozi wa chama hicho hakuwayumbishi bali kunawajenga kisiasa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amezungumza na waandishi wa habari leo na kueleza kuwa suala hilo halitachukua muda mrefu kwenye utekelezaji.
“Hapa tunapoongea Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime, Misiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi,” amesema Dk Mashinji.
Amesema Watanzania wanapaswa kukemea suala hilo kwa kupaza sauti zao zifike mataifa mbalimbali wafahamu ukiukwaji wa sheria.
Post a Comment