Header Ads

test

Masogange Aliniletea Nyodo Wakati Napambana na Dawa za Kulevya - Dk Mwakyembe




Dkt. Harrison Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba ameendelea kufunguka changamoto zilizomkwamisha kudhibiti upitishwaji wa dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam wakati alipokuwa Waziri wa Uchukuzi hadi kuzidiwa kete na Agnes Masogange.

Kupitia kipindi cha Breakfast cha East Africa Waziri Mwakyembe amesimulia kilichotokea wakati alipotaka kumdhibiti binti mmoja aliyedaiwa kupitisha masanduku matano ya ‘materials’ za kutengenezea dawa za kulevya aliyekamatwa nchini Afrika Kusini akitokea Tanzania.
Dkt. Harrison Mwakyembe.
Amesema baada ya kufuatilia sakata lile mbali na kuchukua hatua kwa watu waliomsaidia kupitisha mzigo uwanja wa ndege, aliamua kufanya jitihada za kumkamata binti huyo ili achukuliwe hatua, lakini muda mfupi baada ya binti huyo kurejea nchini, yeye alihamishwa wizara, hivyo kukosa nguvu ya kumshughulikia, hatua iliyofanya binti huyo kumfanyia “nyodo”.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa binti ambaye alikamatwa nchini Afrika Kusini wakati huo kwa madai hayo, na kisha Waziri Mwakyembe kumfuatilia hadi kutimua baadhi ya watumishi wa uwanja huo Mwezi Agosti mwaka 2013 alikuwa ni ‘video queen’ maarufu nchini, Agnes Gerald ‘Masogange’.

Aidha Mwakyembe amesema kijana wake mmoja anayefahamika kwa jina la Jingu ambaye yuko gerezani, anapaswa kuongezewa ulinzi kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa jemedari wa kudhibiti dawa za kulevya uwanjani hapo, lakini baadaye aliundiwa kesi na sasa huko gerezani anakutana na watu ambao wanaweza kumdhuru kutokana na kwamba yeye ndiye aliyesababisha wafungwe.

No comments