Wema Sepetu Atua Rasmi Chadema, Asema Uamuzi Wake ni Sahihi
MSANII maarufu nchini ambaye pia ni Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Isaac Sepetu leo amekihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakati akiongea na wanahabari nyumbani kwa mama yake maeneo ya Sinza, Mori jijini Dar es Salaam.
Yafuatayo ni baadhi ya maneno aliyoyaongea mrembo huyo;
WEMA SEPETU: Ninachokitaka katika nchi yangu ni haki na freedom, naamini kuna watu wengi wapo kwenye nafasi kama niliyonayo mimi, wanaogoga kuchukua maamuzi, kwangu mimi sitarudi nyuma.
WEMA SEPETU: Nimewahi kusema nitakufa nikiwa ndani ya CCM lakini sikujua na ninatamani ningejua zamani, ila sijachelewa na ninaamini uamuzi wangu ni sahihi.
WEMA SEPETU: Nilikipigania chama cha mapinduzi kwa nguvu zangu zote, nafikiri ni zaidi hata ya nguvu zangu za asili, nimelelewa ndani ya CCM.
WEMA SEPETU: Nikiongea vitu vingi nitakuwa naharibu mpango mzima nilitaka kuwahakikishia kuwa kweli nimehama chama, najivunia kuwa memba wa CHADEMA
WEMA SEPETU:Kuna madeni kweli wasanii wenzangu wanadai, nikiwemo mm, ndiyo madeni yapo na wasanii wenzangu wanadai, tumekuwa tukiambiwa tumfuate JK
WEMA SEPETU: Sijahama kwa hasira, kama ingekuwa hasira ningeacha kipindi kile nilipokosa ubunge. Nilikasirika sana lakini sikuhama.
WEMA SEPETU: Sijachukua hata shilingi kutoka kwa CHADEMA, kama ningekuwa nimechukua kaburi la baba yangu lititie, ni uamuzi mgumu lakini niko tayari
WEMA SEPETU: Nimekuwa bize na sijashika simu yangu, natamani nipate muda niingie instagram nikatoe kale kapicha ka CCM nilikokaweka.
Post a Comment