Vannesa Mdee Mikononi Mwa Polisi Kwa Kuhusishwa na Dawa za Kulevya
Jeshi la Polisi Dar es Salaam limemshikilia Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Vennesa Mdee maarufu kama Vee Money kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya.
Mwanasheria wake, Aman Tenga amethibitisha kuwa mteja wake amejisalimisha mwenyewe Kituo Kikuu cha Polisi, kama ilivyoagizwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akitaja majina ya wanaojihusisha mwezi uliopita.
Mwanasheria Tenga pia amethibitisha kuwa Vanessa alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati jina lake likitajwa na Mkuu wa Mkoa. Pia aliongeza kuwa polisi walikwenda nyumbani kwa Vanessa kufanya upekuzi kabla ya kumpeleka kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi.
Post a Comment