Header Ads

test

WAWILI WAFARIKI KATIKA MAANDAMANO YA UCHAGUZI KENYA



Mawe yakiwa yamepangwa barabarani wakati polisi wakiimarisha usalama.

Watu wawili wameuawa wakati wa vurugu akikabiliana na maofisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare, Mji Mkuu wa Nairobi nchini Kenya.


Risasi zikilindima.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa walisikia milindimo ya risasi zikifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo ambayo yalisababisha vifo hivyo.


Polisi wakituliza ghasia.

Afisa Habari wa Shirika la Habari la Uransa, Agence France-Presse (AFP), limeeleza kuwa, waliouawa walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji katika eneo hilo ambao walikuwa wakipambana na kikosi maalum cha kuzuia ghasia hizo.


Hali ilivyokuwa.
”Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi”, alisema ofisa huyo.

Askari wakituliza ghasia.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.

Mataili yakichomwa barabarani.

No comments