Header Ads

test

Simba Yatawala Tuzo za TFF 2021 Dar, Bocco MVP wa Ligi

 


HATIMAYE Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) jana walitoa tuzo za msimu wa 2020-21 kwa wachezaji, makocha, waamuzi na viongozi ambao walifanya vizuri huku Simba ikitawala.

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika jana usiku wa Oktoba 21 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere
uliopo Posta, Dar es salaam.
Tuzo hizo ziligawanyika katika makundi makuu matatu ambayo ni ligi kuu, Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), maarufu kama FA na Ligi ya Wanawake.


Wakati tunaelekea mitamboni,
kuna vipengele ambavyo havikuwa na maswali mengi kama tuzo ya mfungaji bora
ambayo ilikwenda kwa John
Bocco aliyefunga mabao 14.


Tuzo ya timu bingwa ya ligi
kuu na FA ambayo ilikwenda kwa Simba. Lakini kuna vipengele ambavyo viliwaumiza vichwa watu wengi kama tuzo ya beki bora wa msimu, Dickson Job wa Yanga, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wa Simba, huku kura nyingi zikionekana kwenda kwa Tshabalala kutokana na takwimu zake kuwa juu kuliko wengine.


Tuzo ya kipa bora ligi kuu
na FA kura zikiwa nyingi zaidi ya Aishi Manula wa Simba na kuwamwaga wenzake, Harun
Mandanda (Mbeya City),
Jeremiah Kisubi (Prisons), Faroukh Shikhalo (KMC) na Ssetuba James wa Biashara.

 

Tuzo ya timu yenye nidhamu ilikuwa inawaniwa na Coastal Union, Simba na Mwadui, huku Mwadui wakionekana kuwa na nafasi nzuri ya kutwaa tuzo hiyo kutokana na kuwa na kadi chache na kucheza kwa ari hadi mwisho licha ya kushuka daraja mapema.

Tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu na FA ikionekana kumuegemea zaidi John Bocco, huku akiwaacha kwa mbali kidogo Clatous Chama, Mukoko Tonombe, Feisal Salum na Luis Miquissone.

 

Didier Gomes, George Lwandamina na Francis Baraza wakiwania tuzo ya kocha bora, Ramadhan Kayoko, Ahmed Aragija na Emmanuel Mwandembwa wakiwania refa bora.

 

Kilitajwa pia na kikosi bora cha msimu.Kulikuwa na tuzo ya mfungaji bora, kipa bora, golikipa bora, timu bingwa na mchezaji bora chipukizi kwa upande wa
wanawake.

Aisha Masaka akiwa mfungaji bora akitokea Yanga sambamba na Amina Ally wa Yanga akiwa mchezaji bora.Mussa Mgosi wa Simba, Edna Lema wa Yanga na Ally Ally wa Simba wakiwania tuzo ya kocha bora. Ilitolewa tuzo ya heshima ya soka la wanawake pia.

 

Kulikuwepo na tuzo ya Rais wa TFF, tuzo ya mchezaji gwiji na tuzo ya heshima pia. Kiungo bora ligi kuu na FA nazo pia zilitolewa, Clatous Chama, Mukoko Tonombe na Feisal wakichuana.Tuzo nyingine ni mchezaji bora chipukizi ligi kuu, kamishna bora, meneja bora wa uwanja

No comments