IEBC: Mfumo wetu wa matokeo haukudukuliwa
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imesema kuwa mfumo wake wa kutoa matokeo haukudukuliwa kama ilivyodaiwa na upinzani.
Mkurugenzi mkuu wa tume hiyo Ezra Chiloba amesema kuwa madaia yaliotolkewa na mgombea wa upinzani Raila Odinga hayana msingi wowote.
Amesema kuwa tume hiyo imefanya uchunguzi kubaini hayo.
Ameongezea kuwa kufikia sasa wamepokea fomu 29,000 34A na kwamba wanatarajia fomu zote 40,000 kufikia kesho alfajiri.
Vilevile ameongezea kuwa upigaji kura umkamilika katika vituo vyote nchini
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa
- Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 8009175 votes (54.31%)
- Raila Odinga wa ODM ana kura 6608405 votes (44.81%)
Post a Comment